UTAFITI: Uzalishaji mbegu za kiume waporomoka duniani | mwanawakunyumba

Breaking News
Loading...

my ads

Wednesday, 26 July 2017

UTAFITI: Uzalishaji mbegu za kiume waporomoka duniani

Image result for sperm


tafiti mpya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Hebrew-Hadassah Braun cha Jerusalem umebaini kuwa kiwango cha mbegu za kiume kwa wanaume duniani kimepungua kwa zaidi ya asilimia 50.
Image result for sperm


Utafiti huo umeeleza kuwa kiwango na ubora wa mbegu za kiume kimeshuka katika kipindi cha chini ya miaka 40 na hakuna ushahidi kuwa kiwango hicho kitaongezeka.
Hata hivyo utafiti huo umesisitiza kuwa kiwango na idadi ya mbegu za kiume kimeshuka zaidi kwa wanaume wa nchi za Magharibi.
Pia imeelezwa kuwa kushuka kwa ubora na idadi ni tishio kwa uwepo wa watu duniani.
“Utafiti huu unawapa wasomi kazi kubwa zaidi hasa kwani idadi ya mbegu za kiume na afya ya binadamu ni muhimu zaidi. Wasomi sasa wanatakiwa kuchunguza chanzo cha kushuka huko kwa idadi ya mbegu za kiume na namna ya kutatua tatizo hilo,” amesema Dk Hagai Levine.
Profesa Hagai ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mazingira na Afya wa Chuo cha Hebrew, amefanya utafiti huo kwa kushirikiana na Profesa Hannah Swan wa Chuo Kikuu cha New York kitengo cha Afya ya Jamii.
Madaktari wengine waliohusika katika utafiti huo ni wa Brazil, Denmark, Israel, Hispania na Marekani. Utafiti huo umefafanua zaidi kuwa kiwango na idadi ya mbegu za kiume ni kipimo sahihi cha uwezo wa kuzalisha wa mwanaume.

google+

linkedin

BONGOCLICK1blog
  • INAKULETEA NAFASI ZA MATANGAZO YA MASOMO KWA NGAZI ZOTE, NAFASI ZA KAZI KWA NGAZI ZOTE, HABARI MPYA NA PIA TUNATOA USHAURI NA KUPOKEA MATANGAZO YA KITAALUMA KAZI NA HABARI, WASILIANA NASI KUPITIA 0655065855 MATANGAZO YA TAALUMA KWA SH.5000 PER DAY AMBAPO LITAWAFIKIA ZAIDI YA WATU 100,000 KWA SIKU Read More

    0 comments:

    POST A COMMENT