MUDA ATAKAOKAA NJE PAUL POGBA BAADA YA KUTHIBITISHWA KUA ANAHITAJIKA KUFANYIWA UPASUAJI | mwanawakunyumba

Breaking News
Loading...

my ads

Tuesday, 26 September 2017

MUDA ATAKAOKAA NJE PAUL POGBA BAADA YA KUTHIBITISHWA KUA ANAHITAJIKA KUFANYIWA UPASUAJI

Mchezaji ghali zaidi katika kikosi cha Man United Paul Pogba kuna uwezekano akawa nje ya uwanja kwa muda mrefu zaidi kutokana na jeraha lake la hamstring kuripotiwa kuwa linahitaji kufanyiwa upasuaji ili kutibu tatizo na itamfanya awe nje ya uwanja kwa wiki sita zaidi.
Paul Pogba aliumia mapema mwanzo wa mwezi huu wakati wa mchezo wa UEFA Champions League kati ya Man United dhidi ya FC Basel, kwa mujibu wa doctor Sakari Orava anayemsimamia Pogba na kuhakikisha anarudi kuwa sawa, anadai staa huyo bado hajafanyiwa upasuaji.
Staa huyo wa Man United ambaye ni moja kati ya wachezaji muhimu katika kikosi cha Man United, hadi sasa baada ya kuumia Pogba amekosa michezo ya Ligi Kuu England dhidi ya Everton, Southampton  na mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya Burton Albion.

google+

linkedin

BONGOCLICK1blog
  • INAKULETEA NAFASI ZA MATANGAZO YA MASOMO KWA NGAZI ZOTE, NAFASI ZA KAZI KWA NGAZI ZOTE, HABARI MPYA NA PIA TUNATOA USHAURI NA KUPOKEA MATANGAZO YA KITAALUMA KAZI NA HABARI, WASILIANA NASI KUPITIA 0655065855 MATANGAZO YA TAALUMA KWA SH.5000 PER DAY AMBAPO LITAWAFIKIA ZAIDI YA WATU 100,000 KWA SIKU Read More

    0 comments:

    POST A COMMENT