Tuhuma za kauli za kichochezi zamrudisha Mhe Lissu rumande
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mbunge wa
Singida Mashariki, Mhe Tundu Lissu amefikishwa katika Mahakama ya
Kisutu, Dar es Salaam na kusomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi.

Mhe Tundu Lissu katikati akirudishwa rumande.
Imedaiwa kuwa maneno hayo yalikuwa na lengo ya kuleta chuki dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alipotakiwa kukubali ama kukataa makosa hayo mbele ya Hakimu Mashauri, Lissu amesema kusema kweli haijawahi kuwa kosa la jinai kwa maneno aliyotamka.
Mhe Lissu amenyimwa dhamana na kurudishwa rumande mpaka Tar 27 Julai kesi yake itakaposikilizwa tena.
0 comments:
POST A COMMENT