mwanawakunyumba

mwanawakunyumba

Breaking News
Loading...

my ads

Latest Post

Tuesday, 3 October 2017

KWA MARA YA KWANZA HASHEEM THABEET KUSHUKA DIMBANI KATIKA TIMU YAKE MPYA

Mtanzania, Hasheem Thabeet ambaye amesajiliwa na klabu ya Yokohama B inayoshiriki Ligi Kuu ya mchezo wa mpira wa kikapu nchini Japan ‘B1 League’ anatarajia kuanza kutupa karata yake ya kwanza dhidi ya timu ya Levanga Hokkaido katika dimba la kimataifa la Yokohama ‘Yokohama International Arena Pool’.


Thabeet atacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Levanga Hokkaido Oktoba 7 ya wiki hii ikiwa ni tangu alipojiunga na timu hiyo Septemba 28 mwaka huu.

BAADA YA HASHEEM KUACHANA NA NBA AELEKEA CHINA

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Tanzania Hasheem Thabeet ambaye ni mchezaji wazamani wa klabu ya Oklahoma City Thunder inayoshiriki ligi ya Marekani ‘NBA’, amecheza jumla ya michezo 224 NBA ikiwa ni sawa na wastani wa pointi 2.1 na mitupo 2.6 ‘rebounds.’

Tuesday, 26 September 2017

MUDA ATAKAOKAA NJE PAUL POGBA BAADA YA KUTHIBITISHWA KUA ANAHITAJIKA KUFANYIWA UPASUAJI

Mchezaji ghali zaidi katika kikosi cha Man United Paul Pogba kuna uwezekano akawa nje ya uwanja kwa muda mrefu zaidi kutokana na jeraha lake la hamstring kuripotiwa kuwa linahitaji kufanyiwa upasuaji ili kutibu tatizo na itamfanya awe nje ya uwanja kwa wiki sita zaidi.
Paul Pogba aliumia mapema mwanzo wa mwezi huu wakati wa mchezo wa UEFA Champions League kati ya Man United dhidi ya FC Basel, kwa mujibu wa doctor Sakari Orava anayemsimamia Pogba na kuhakikisha anarudi kuwa sawa, anadai staa huyo bado hajafanyiwa upasuaji.
Staa huyo wa Man United ambaye ni moja kati ya wachezaji muhimu katika kikosi cha Man United, hadi sasa baada ya kuumia Pogba amekosa michezo ya Ligi Kuu England dhidi ya Everton, Southampton  na mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya Burton Albion.

YALIYOJIRI BAADA YA DIEGO COSTA KUONDOKA CHELSEA.

Mwanasoka wa kimataifa wa Hispania mwenye asili ya Brazil Diego Costa usiku wa September 26 2017 amefanikiwa kusaini mkataba wa kurejea Atletico Madrid kwa mara nyingine tena akitokea Chelsea.

Diego Costa tayari amepewa jezi namba 18 na Atletico Madrid hivyo tutaanza kumuona akiivaa rasmi mwezi January 1 atakapoanza kuichezea katika mechi za mashindano, Costa amesaini mkataba baada ya kufuzu vipimo vya afya alivyofanyiwa Jumamosi na Jumatatu.

Hata hivyo Diego Costa atajiunga na timu na kuanza kufanya mazoezi lakini hatokuwa na nafasi ya kuichezea hadi dirisha la usajili la majira ya baridi la January litakapofunguliwa, kama utakuwa unakumbuka vizuri Costa alijiunga na Chelsea 2014 akitokea Atletico Madrid aliyodumu nayo kwa miaka minne.

Thursday, 10 August 2017

IJUE SABABU YA KUVUNJIKA KWA NDOA YA NUH MZIWANDA NA NAWAL

Image result for NUH MZIWANDA NA NAWALImage result for NUH MZIWANDA NA NAWAL
Baada ya ndoa ya Nawal na Mwimbaji Nuh Mziwanda kuvunjika na kila mmoja akishindwa kuweka wazi sababu ya kuvunjika kwa ndoa hiyo huku Nawal akiolewa na mwanaume mwingine, sasa new stori ni kwamba mshenga wa ndoa hiyo amefunguka.
Kupitia kipindi cha The Weekend Chat Show ya Clouds TV Mshenga wa ndoa hiyo anayefahamika kama HK ameeleza hajui sababu kubwa iliyopelekea kuvunjika kwa ndoa hiyo bali ni mvutano wa masuala ya kidini kati ya Nawal na familia ya Nuh Mziwanda hasa mama mzazi wa Nuh aliyedai haitambui ndoa hiyo. 

>>>”Ukiacha tofauti zao zilizokuwa zikitokea, kilichotokea sasa hivi wamekuwa wakivutana sana Nuh alikuwa anataka Nawal akakae kwa mama yake na Nawal hataki kukaa kwa mama yake Nuh kwa sababu mama yake Nuh anasema haitambui ndoa yao kwa sababu mwanae ni Mkristo na hajui kwa nini kabadilisha dini.
“Kwa hiyo, hiyo ndoa haitambui. Hiyo ndio kesi kubwa nilikuwa nikivutana nayo sana mpaka dakika ya mwisho niliongea na mama yake Nuh kwenye simu akanambia mwanangu umefanya makosa sana kumuozesha mwanangu bila mimi mwenyewe kujua.” – HK Hypeman.

HUZUNI KUBWA KWA MASHABIKI WA ARSENAL

LONDON, ENGLAND - AUGUST 06: Alexis Sanchez of Arsenal applauds the Arsenal fans during the The FA Community Shield between Chelsea and Arsenal at Wembley Stadium on August 6, 2017 in London, England.  (Photo by Robbie Jay Barratt - AMA/Getty Images)Arsenal inaenda kuikaribisha timu ya leicester city katika uwanja wake wa nyumbani Emirates stadium siku ya kesho tar 11/8/2017, timu hizo zote mbili  zitaingia uwanjani hapo bila wachezaji wao muhimu, katika timu ya arsenal wataenda kumkosa mchezaji wao mashuhuri kabisa Alexis Sanchez, Mesuit Ozil na Aaron Ramsey ambao walipata majeraha katika mechi dhidi ya chelsea. Na katika timu pinzani leicester city wataingia uwanjani hapo bila mchezaji wao playmaker Danny Drinkwater.

Wednesday, 9 August 2017

MRITHI WA NEYMAR JR BARCELONA HUYU HAPA

Hatimae club hyo ya barcelona imefanikiwa kumnyakua mshambuliaji mwenye uraia wa brazil alietokea katika club ya liverpool ambae ndo atakaeweza kuziba pengo la mchezaji machachari neymar jr kuelekea katika club ya psg mapema mwezi huu

Wednesday, 2 August 2017

NEYMAR JR KUTAMBULISHWA LEO KATIKA CLUB YAKE MPYA

Kwa mashabiki wa klabu ya Barcelona huenda wasiamini tetesi za mshambuliaji wao Mbrazil, Neymar Jr kuwa ameitosa klabu yake na kuhamia kwa matajiri wa Ufaransa, Paris Saint-Germain, ukweli ni kwamba dili hilo ni asilimia 98 limeshatiki kinachosubiriwa ni masaa tu atangazwe.
Tokeo la picha la Neymar usa tour
Neymar Jr

Kwa mujibu wa magazeti makubwa nchini Ufaransa kama L’Équipe na Europe 1 yametangaza kuwa Neymar jana jumanne anaenda Doha, Qatar kuonana na Rais wa klabu hiyo Nasser Al-Khelaifi na kufanyiwa vipimo vya afya.
Zoezi la kumtambulisha na kumtangaza Neymar linatarajiwa kufanyika leo, jumatano tar 2 Agosti kwa mbwembwe ndani ya jiji la Paris nchini Ufaransa ambapo maelfu ya mashabiki wa klabu hiyo watahudhuria kwenye uwanja wa klabu hiyo.
Kwa mujibu wa gazeti la L’Équipe taarifa zinaeleza kuwa viongozi wa klabu hiyo wapo kwenye mazungumzo na Meya wa jiji hilo kuomba kibali cha kuweka picha kubwa ya Neymar kwenye mnara maarufu zaidi duniani ulio katikati ya jiji hilo ujulikanao kwa jina la  Eiffel kama walivyowahi kufanya kwa Zlatan Ibrahimovic walivyomsajili akitokea Barcelona.

Uhamisho wa Neymar kutoka Barcelona umeripotiwa kuwa ni wa Euro Milioni 193 na kama itatokea utakuwa ndio usajili wa ghali zaidi duniani kuwahi kutokea katika historia ya mpira wa miguu.
Hata hivyo taarifa hizo za Neymar kuhama Barcelona zinashika kasi kwa kile kinachoonekana kuwa klabu hiyo imeshindwa kumlipa baba yake mzazi na Neymar, Neymar Sernior ambaye ndiye meneja wake kiasi cha Euro Milioni 26 kama masharti ya mkataba yalivyoeleza.
Katika mkataba alioingia na Barcelona akitokea Klabu ya Santos ya Brazil, unaeleza kuwa kama Neymar akiongeza mkataba mpya na Barcelona, basi baba yake huyo ambaye ni meneja wake anapaswa kulipa kitita cha euro milioni 26.