IJUE SABABU YA KUVUNJIKA KWA NDOA YA NUH MZIWANDA NA NAWAL | mwanawakunyumba

Breaking News
Loading...

my ads

Thursday, 10 August 2017

IJUE SABABU YA KUVUNJIKA KWA NDOA YA NUH MZIWANDA NA NAWAL

Image result for NUH MZIWANDA NA NAWALImage result for NUH MZIWANDA NA NAWAL
Baada ya ndoa ya Nawal na Mwimbaji Nuh Mziwanda kuvunjika na kila mmoja akishindwa kuweka wazi sababu ya kuvunjika kwa ndoa hiyo huku Nawal akiolewa na mwanaume mwingine, sasa new stori ni kwamba mshenga wa ndoa hiyo amefunguka.
Kupitia kipindi cha The Weekend Chat Show ya Clouds TV Mshenga wa ndoa hiyo anayefahamika kama HK ameeleza hajui sababu kubwa iliyopelekea kuvunjika kwa ndoa hiyo bali ni mvutano wa masuala ya kidini kati ya Nawal na familia ya Nuh Mziwanda hasa mama mzazi wa Nuh aliyedai haitambui ndoa hiyo. 

>>>”Ukiacha tofauti zao zilizokuwa zikitokea, kilichotokea sasa hivi wamekuwa wakivutana sana Nuh alikuwa anataka Nawal akakae kwa mama yake na Nawal hataki kukaa kwa mama yake Nuh kwa sababu mama yake Nuh anasema haitambui ndoa yao kwa sababu mwanae ni Mkristo na hajui kwa nini kabadilisha dini.
“Kwa hiyo, hiyo ndoa haitambui. Hiyo ndio kesi kubwa nilikuwa nikivutana nayo sana mpaka dakika ya mwisho niliongea na mama yake Nuh kwenye simu akanambia mwanangu umefanya makosa sana kumuozesha mwanangu bila mimi mwenyewe kujua.” – HK Hypeman.

google+

linkedin

BONGOCLICK1blog
  • INAKULETEA NAFASI ZA MATANGAZO YA MASOMO KWA NGAZI ZOTE, NAFASI ZA KAZI KWA NGAZI ZOTE, HABARI MPYA NA PIA TUNATOA USHAURI NA KUPOKEA MATANGAZO YA KITAALUMA KAZI NA HABARI, WASILIANA NASI KUPITIA 0655065855 MATANGAZO YA TAALUMA KWA SH.5000 PER DAY AMBAPO LITAWAFIKIA ZAIDI YA WATU 100,000 KWA SIKU Read More

    0 comments:

    POST A COMMENT