KWA MARA YA KWANZA HASHEEM THABEET KUSHUKA DIMBANI KATIKA TIMU YAKE MPYA | mwanawakunyumba

Breaking News
Loading...

my ads

Tuesday, 3 October 2017

KWA MARA YA KWANZA HASHEEM THABEET KUSHUKA DIMBANI KATIKA TIMU YAKE MPYA

Mtanzania, Hasheem Thabeet ambaye amesajiliwa na klabu ya Yokohama B inayoshiriki Ligi Kuu ya mchezo wa mpira wa kikapu nchini Japan ‘B1 League’ anatarajia kuanza kutupa karata yake ya kwanza dhidi ya timu ya Levanga Hokkaido katika dimba la kimataifa la Yokohama ‘Yokohama International Arena Pool’.


Thabeet atacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Levanga Hokkaido Oktoba 7 ya wiki hii ikiwa ni tangu alipojiunga na timu hiyo Septemba 28 mwaka huu.

BAADA YA HASHEEM KUACHANA NA NBA AELEKEA CHINA

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Tanzania Hasheem Thabeet ambaye ni mchezaji wazamani wa klabu ya Oklahoma City Thunder inayoshiriki ligi ya Marekani ‘NBA’, amecheza jumla ya michezo 224 NBA ikiwa ni sawa na wastani wa pointi 2.1 na mitupo 2.6 ‘rebounds.’

google+

linkedin

BONGOCLICK1blog
  • INAKULETEA NAFASI ZA MATANGAZO YA MASOMO KWA NGAZI ZOTE, NAFASI ZA KAZI KWA NGAZI ZOTE, HABARI MPYA NA PIA TUNATOA USHAURI NA KUPOKEA MATANGAZO YA KITAALUMA KAZI NA HABARI, WASILIANA NASI KUPITIA 0655065855 MATANGAZO YA TAALUMA KWA SH.5000 PER DAY AMBAPO LITAWAFIKIA ZAIDI YA WATU 100,000 KWA SIKU Read More

    0 comments:

    POST A COMMENT